Ashirafu Awadh na Amiry Luwiso waliokua wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Tsh. Milioni 280 wamehukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya Tsh. 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka.
Ashirafu Awadh na Amiry Luwiso waliokua wakikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Tsh. Milioni 280 wamehukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya Tsh. 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka. Hukumu imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya washtakiwa kutimiza masharti ya makubaliano ya kukiri kosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)