Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliomua mwanajeshi kwenye mashamba ya katani wahukumiwa kunyongwa

Newslite1663763403523 Waliomua mwanajeshi wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro imewahukumu kunyongwa hadi kufa Watu watatu kwa kosa la kumuua Leonard Yamakwa ambaye alikuwa Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Akisoma hukumu hiyo yenye shauri namba 6 ya mwaka 2020 Msajili wa Mahakama ya Rufani Silivester Kahinda amewataja waliohukumiwa kuwa ni Charles, Hassan Athuman na Alfred Dotto ambapo amesema Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo May 25, 2019 .

Amesema Washtakiwa hao siku ya tukio majira ya saa kumi na mbili za jioni walimkuta Leonard akiwa na Mpenzi wake katika mashamba ya Mikonge Tungi Manispaa ya Morogoro wakifanya mapenzi ndipo wakamtaka aondoke peke yake na aache pikipiki na Mwanamke jambo ambalo Leonard alikataa kutii .

Baada ya Leonard kukataa Watuhumiwa walimshambulia na vitu vizito kichwani hadi kupoteza maisha kisha kumchukua Mwanamke huyo na kumbaka kila mmoja kwa wakati wake kisha waliondoka na pikipiki na simu za Leonard ambazo zilikuwa moja ya vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani.

Washitakiwa wanadaiwa kutenda kosa la mauaji kinyume na kifungu cha 196 na 197 kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002 na baada ya Mahakama kupitia ushahidi uliotolewa na Mashahidi 16 na vielelezo 10 umewachia huru Washitakiwa 6 waliokuwa wanashitakiwa katika kesi hiyo ambao ni Juma Said ,Yusuph Hussein, Mbaya Edward, Manambo Michael, Rehema Kibwana na Daudi Chilongo huku washitakiwa wengine watatu wakihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live