Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliolawiti wahukumiwa vifungo jela, kulipa fidia

Aweitipic Data Waliolawiti wahukumiwa vifungo jela, kulipa fidia

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi imemhukumu Shahaa mkazi wa Kilwa Masoko kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumlawiti mtoto wa Shule ya Msingi Kilwa.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo,  Innocent Sotter amesema amemtia hatiani mshtakiwa kwa kosa hilo chini ya kifungu namba 154 (1) (2) kanuni ya adhabu sura ya 16 ya toleo la mwaka 2019

Sotter  amesema kuwa  mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa  na upande wa mlalamikaji mahakamani  hapo na  kumtia hatiani bila na shaka yeyote mshtakiwa  baada ya ushahidi uliotolewa na mashahidi wa pande zote mbili.

Wakati huo huo,  Rajabu Litanda amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya Sh2 milioni  kwa kosa la kulawiti.

Hakimu mfawidhi Mahakama ya Wilaya Kilwa,  Alice Mkasela amesema  Litanda amekutwa na adhabu hiyo  kwa mujibu wa kifungu 154(1)(2) kwa mujibu wa kanuni ya adhabu sura 16 ilifanyiwa marekebisho Mwaka  2019.

Amesema Juni 26, 2021 kijiji cha Banduka Kilwa mtuhumiwa akiwa ameongoza zana mlalamikaji wakitokea kunywa pombe alipiga ngwala  na kumlawiti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live