Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokuwa wafanyakazi wa TBL kukata rufaa Mahakama Kuu

HUKUMU Waliokuwa wafanyakazi wa TBL kukata rufaa Mahakama Kuu

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) zaidi ya 500 wanatarajia kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania wakipinga maamuzi yaliyotolewa na Tume ya Usulushishi baini yao na Kampuni ya Bia Tanzania ikiijumuisha Mfuko wa Hisa wa Wafanyakazi wa Kampuni hiyo.

Pia, wanapinga kesi hiyo kuendesha kwa muda wa miaka minne kinyume na sheria inayoelekeza ndani ya miezi sita shauri hilo linatakiwa liwe limeisha lakini imekuwa tofauti.

Waliokuwa wafanyakazi hao zaidi ya 1,200 walifungua shauri la madai katika tume hiyo wakidai watambuliwe kuwa ni miongoni mwa wanufaika wa mazao ya mfuko wa hisa na kwamba wanastahili kupata mgawo katika kipindi walichokuwa kazini waliutumikia mfuko huo.

Katika Shauri hilo Jaji mstaafu Twaib Fauz alitoa uamuzi mnamo Septemba 14, 2023 kuwa waliokuwa wafanyakazi kati ya mwaka 1998 hadi Novemba,23,2011 hawatalipwa hisa za mfuko huo kwa kigezo kuwa ziliisha na kwamba wafanyakazi hao walishalipwa.

Katika hukumu hiyo inaeleza kuwa kipindi cha mwaka 1998 hadi Novemba 2011 mfuko huo ulitoa hisa kwa wafanyakazi hao huku sheria na kanuni zilifuatwa ambapo hisa za awali 1,200,000 ziliisha.

Fauz alisema katika hukumu hiyo wanaostahili kulipwa hisa hizo ni wafanyakazi waliokuwepo kazini kuanzia Novemba 24, 2011 hadi Desemba 30, 2017.

Wakili wa kujitegemea wa kundi hilo, Dk Hamisi Masoud alidai maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo waliokuwa wafanyakazi hao wamewakoseshwa haki ya mgawo wa fedha hizo kwa sababu zisizokuwa za msingi.

"Hoja iliyopo kwa nini wawabague wakati wote walikuwa ni wafanyakazi wakiutumikia mfuko huo kwa nyakati tofauti tunatarajia kukata rufaa kwa sababu sheria ni tafsiri kila mtu anaweza kuitafsiri hivyo hoja za msingi ni kwamba tume hii lilitakiwa wazingatie vyema shauri hili kwenye maamuzi yake ili haki itendeke kwa wote," amedai Dk Masoud.

Dk Masoud alidai mfuko huo ulivunjwa kinyemela mnamo Desemba 2017 kupitia bodi ya wakurugenzi iligawa mabilioni fedha nje ya utaratibu unaoungoza mfuko huo jambo lililopelekea Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kuufunga mfuko huo mara moja kuzuia ugawaji holela wa fedha hizo.

Alidai mfuko huo ulipaswa kuwepo kwa kipindi cha miaka 20 kwa mujibu wa sheria na kanuni zake hivyo hapakuwepo na sababu za msingi ya kuwagawa wafanyakazi hao kwa makundi mawili moja likipata na jingine kukosa ndani ya kipindi kimoja.

Akizungumzia hukumu hiyo Mwenyekiti wa kundi hilo lilikosa mgao wa hisa za mfuko huo, Mohamed Lemu alidai kuwa maamuzi yaliyotolewa na baraza hilo hayakuzingatia ushahidi uliowasilishwa kwenye baraza hilo hivyo wanatarajia kukata rufaa ili haki itendeke.

Lema anadai kuwa katika hukumu hiyo inaeleza kipindi cha mwaka 1998 hadi Novemba 2011 mfuko huo ulitoa hisa kwa wafanyakazi hao ambazo zilikuwa 1,200,000 kwa kufuata sheria na kanuni za mfuko huo ambazo ziliisha.

"Ukweli ni kuwa kwa kipindi hicho mfuko uliwapa hisa watu chini ya 40 sawa na asilimia 1.4 wengi wao wakiwa ni viongozi waandamizi wa Kampuni TBL huku wafanyakazi wa chini waliokuwepo kwenye viwanda vya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya wanakadiliwa kuwa i kati ya 2,600 hadi 3,000.

Wafanyakazi 40 waliopata hisa kwa kipindi chote cha uhai wa mfuko huo hawakufuata utaratibu ulioanishwa kwenye katiba ya mfuko kulikuwa na ukiukwaji mkubwa kwa kuwa baada ya kuanzishwa wafanyakazi hao hawakuambiwa na kuonyeshwa katiba ya mfuko huo na tararibu zake za kujiunga.

Alidai kuwa katiba (Trust Deed) yenyewe ina walakini mkubwa kwa kuruhusu wizi, kugushi na uzembe ambavyo kwa pamoja ni makosa ya jinai na inapingana na sheria za nchi.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo inadaiwa kuwa hisa zilizotengwa kwa ajili ya wafanyakazi hao kwenye mfuko huo zilikuwa 5,898,596 sawa na asilimia mbili ya hisa za TBL ambapo hadi kufikia mwaka 2017 thamani yake iliikuwa Sh83 billioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live