Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokutwa na tausi wa Ikulu wahukumiwa kulipa Sh6.8 milioni

82351 Tausipic Waliokutwa na tausi wa Ikulu wahukumiwa kulipa Sh6.8 milioni

Thu, 31 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu watatu wanaodaiwa kukutwa na ndege aina ya tausi wa Ikulu wamehukumiwa kulipa fidia zaidi ya Sh6.8 milioni baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na nyara za Serikali bila kibali.

Mbali na kutakiwa kulipa faini hiyo, wametakiwa kutofanya makosa katika kipindi cha miezi sita huku ndege hao wakirejeshwa serikalini.

Washtakiwa hao ni David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 30, 2019 na Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu, Salum Ally aliyesema kuwa amezingatia masharti ya makubaliano ya washtakiwa hao waliokubali kuilipa Serikali fidia ya zaidi ya Sh6.8 milioni.

"Mahakama imewaachia huru kwa masharti kwamba washtakiwa wasitende kosa lolote ndani ya miezi sita, iwapo watatenda kosa katika kipindi hicho wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria," amesema Ally.

Awali mahakama hiyo iliwafutia mashtaka manne likiwemo  la kuongoza mtandao wa uhalifu na

Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya washtakiwa hao, kuiomba mahakama kutoa  adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwa wengine.

Baada ya maelezo hayo, washtakiwa waliiomba mahakama isiwape adhabu kwa kuwa ni kosa lao la kwanza na wanafamilia zinazowategemea.

Kati ya Juni Mosi, 2015 na Oktoba 14, 2019 maeneo jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walikutwa na nyara za Serikali ambazo ni ndege watatu aina ya tausi wenye thamani ya zaidi ya Sh3.4 milioni  bila ya kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz