Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokamatwa na vifungashio haramu kukiona

C0390fbfa83dfa33a4b597286f4ce36f Waliokamatwa na vifungashio haramu kukiona

Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo ameagiza kuchukuliwa hatua kali kwa watu waliokamatwa na shehena ya vifungashio vilivyopigwa marufuku na serikali.

Jafo ametoa kauli hiyo juzi baada ya kushuhudia magunia 40 na katoni 16 za vifungashio vilivyokamatwa wakati wa msako uliofanywa soko kuu Mwanza.

Akizungumza, Waziri Jafo alisema endapo vifungashio hivyo visingekamatwa vingesambaa mitaani na kutumiwa na walaji na kuendeleza uchafuzi wa mazingira.

“Serikali ilishatoa tamko kuwa mwisho wa vifungashio hivi ni Aprili 8… nina imani watafikishwa haraka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,”alisisitiza.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne alisema ushirikiano wa pamoja kati ya vyombo vya dola na taasisi zingine ikiwemo Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC) ndio umeleta mafanikio hayo.

Meneja wa NEMC wa Kanda ya Ziwa, Redempta Samuel aliwataka wananchi kuacha mara moja kutumia mifuko na vifungashio vilivyopigwa marufu na serikali kuepuka madhara.

Kwa mujibu wa kanuni ya 8 ya Katazo la Mifuko ya Plastiki ambayo inataja makosa matano ya kuzalisha, kuingiza, kusambaza, kuuza na kutumia mifuko iliyokatazwa adhabu yake ni faini ya 30,000 hadi Sh bilioni 10 au kifugo hadi miaka miwili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz