Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokamatwa JNIA na dawa za kulevya wasomewa mashtaka

Waliokamatwapic Data Waliokamatwa JNIA na dawa za kulevya wasomewa mashtaka

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Watuhumiwa wawili waliokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jullius Nyerere (JNIA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini wakikabiliwa na makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

Washitakiwa hao, Said Shewale na Salum Athman, ambao walikamatwa tofauti tofauti uwanjani hapo, wamefikishwa mahakamani leo mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Romuli Mbuya wakituhumiwa kusafirisha jumla ya kilo 7.45 za Heroin.

Akimsomea kila mshitakiwa shitaka lake leo Desemba 17,2021, wakili wa Serikali kutoka ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS), Yusuph Aboud alidai mshitakiwa Shewale alikamatwa uwanjani hapo Novemba 25 akisafirisha kilo 3.85 za dawa hizo.

Kuhusu mshitakiwa Athman, wakili Aboud alidai kuwa mshitakiwa huyo naye alikamatwa maeneo hayo hayo akisafirisha kilo 3.6 za dawa hizo za kulevya.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mbuya alisema shtaka hilo ni la uhujumu uchumi na washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote na washitakiwa wamepelekwa gerezani hadi Desemba29, 2021 kesi itakapotajwa tena.

Wakili Aboud ameambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz