Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walioiba gari Arusha wanaswa

MASEJOOOOOOOOOOOO Walioiba gari Arusha wanaswa

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watuhumiwa wanne kwa kosa la kuiba gari moja aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili IT 3CD50343065 ambapo liliwekewa namba bandia za usajili wa Nchi jirani KDA 222H kwa lengo la kuuzwa jijini Arusha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo ameongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kubaini mtandao mzima

Aidha Wananchi wa jiji la Arusha wamehimizwa kutunza amani na utilivu wa jiji hilo ambalo Lina sifa ya kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya Nchi ikiwa ni sifa ya kuwa na amani na utulivu miongoni mwa majiji hapa Nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo akizungumza kuelekea sikukuu ya Mwaka mpya 2023 amewataka wananchi wa mkoa huo kufuata maelekezo yanayotolewa na serikal na Jeshi hilo ili kulinda heshima ya jiji hilo hapa Nchini

Kamanda Masejo pia amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la mvua nyingi katika Mkoa wa Arusha kitendo kilichopekea madhara kwa wananchi ambapo amewataka wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari.

Aidha ACP Masejo amebainisha kuwa katika mvua zinazoendelea kunyesha zimepekea madhara na kusabisha vifo vya watu watatu ikwemo kijana mmoja aitwaje Baraka mwenye umri wa miaka (17) mwanafunzi ambaye alichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live