Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliohusika na Mauaji Tanga Kusakwa Nyumba kwa Nyumba

ADAM MALIMA Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Tanga Adam Malima, amesema atahakikisha kila aliyeshiriki kwenye mauaji wa watu saba wilayani Kilindi anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea kijiji cha Kibirashi wilayani humo mahali ambapo yametokea mauwaji hayo Januar1 31, 2022.

Amesema Serikali haitakubali kuona wananchi wake wanateseka kutokana na upotevu wa amani unaofanywa na baadhi ya watu.

"Nasema serikali hailali ipo macho muda wote na tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake,"- amesema Adam Malima.

Mpaka sasa waliofariki dunia ni watu saba wakiwemo wawili wa familia moja,ambao ni mama na mtoto wa miaka kumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live