Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliogawana mifugo ya watuhumiwa matatani

Mifugo Ya Ngombe 620x308 Waliogawana mifugo ya watuhumiwa matatani

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Habarileo

JESHI la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu 10 wakiwemo wazee wa kimila maarufu kama Ndagashida na viongozi wa ulinzi wa jadi maarufu sungusungu kwa tuhuma za kuchukua mifugo kwenye familia za watuhumiwa wa kesi ya mauaji na kugawana.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mkoani humo, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu, Blasious Chatanda amesema Februari 2023 kulitokea tukio la mauaji ya mfanyabiashara, William Fumbuka (39) katika Kijiji cha Bukundi, wilayani Meatu.

Chanzo cha kifo chake kilibainika kuwa kulikuwepo na mgogoro wa umiliki wa ardhi inayokadiriwa kufikia ekari 2,500 ambayo ilielezwa kuwa Fumbuka alizitumia kuzikodisha.

Kamanda Chatanda alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita na kuwafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Meatu ndipo viongozi hao wakarudi na kuchukua mifugo katika familia hizo na kugawana kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

“Kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo katika familia hiyo, watuhumiwa walipanga mipango ya kumuua Fumbuka na walitekeleza tukio hilo na hadi sasa tayari watuhumiwa wa tukio hilo wako mikononi mwa Jeshi la Polisi tayari kwa taratibu za kuwafikisha mahakamani zikiendelea,” alisema.

Chanzo: Habarileo