Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliofika Kisutu kwenye kesi ya Mbowe wakamatwa

CHADEMA KISUTU 3.jpeg?fit=854%2C480&ssl=1 Polisi wakiwakamata wafuasi wa CHADEMA

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Wanachama hao waliokuwa wamefika kwaajili ya kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye hata hivyo hakufikishwa mahakamani walikamatwa baada ya kutoa mabango yenye jumbe mbalimbali na kuanza kuimba.

Askari waliokuwa kwenye magari mawili waliteremka kisha kuwazunguka na kuwakamata baadhi yao na wengine kufanikiwa kukimbia

Mbowe ambaye alifikishwa mahakamani hapo, Julai 26, 2021 anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama za kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi, huku wenzake watatu wao wakikabiliwa na mashtaka saba.

Chanzo: globalpublishers.co.tz