Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walinzi GGM wadaiwa kumuua mwananchi

23517 WALINZI+PIC TanzaniaWeb

Mon, 22 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Walinzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwananchi aliyeingia kwa njia za panya katika mgodi huo.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 22, 2018 Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Mengineyo Mabula (19) mkazi wa Samina mjini Geita.

Amesema mauaji hayo yalitokea wakati marehemu na wenzake tisa walipoingia mgodini usiku wa kuamkia Oktoba 21, 2018 kwa lengo la kuiba mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu.

Kamanda Mwabulambo amesema kwamba kutokana na uvamizi huo walinzi wa GGM walilazimika kutumia silaha za moto kutokana na upinzani waliokuwa wanakabiliana nao.

Alisema marehemu alijeruhiwa na risasi tumboni na kifuani na kwamba polisi wanachunguza aina ya silaha iliyotumika.

Chanzo: mwananchi.co.tz