Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu wawili jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi mmoja

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iramba. Walimu wawili wa Shule ya Sekondari Kizaga Wilaya ya Iramba mkoani wa Singida wamehukumiwa kutumikia kifungo gerezani miaka 30 kila moja baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka kwa nyakati tofauti mwanafunzi wao mweye umri wa miaka 15.

Walimu waliokutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi huyo wa kidato cha pili ni Ernest Emmanuel (25) na Onesmo Bida (28) ambao hukumu yao imetolewa hivi karibuni.

Pia, Ally Pandu ambaye ni mwalimu anatuhumiwa kumbana mwanafunzi huyo kesi yake inaendelea mahakamani hapo huku Mahakama hiyo ikiagiza mwalimu mwingine Keneth Komba asakwe na afikishwe mahakamani kujibu shitaka kama la wenzake.

Walimu wote hao wanne wanatuhumiwa kumgeuza mwanafunzi huyo kuwa kama mpira wa miguu kwani walikuwa wakifahamiana katika kutenda kosa hilo.

Mwendesha mashitaka wa Serikali, Lyoba Mkambala alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba, Makwaya Charles kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti tofauti kati ya  Machi 2, 2018 hadi mwanzoni mwa 2019.

Alisema mshitakiwa Ernest Emmanuel alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada wa mwanafunzi wake.

Pia Soma

Advertisement
Mkambala alisema Machi 20, 2018 saa 2 usiku, mwanafunzi huyo alikwenda nyumbani kwa shemeji yake Emmanuel kwa lengo la kuangalia filamu mbalimbali.

“Baada ya kumaliza kuangalia ‘movie’ mwanafunzi huyo aliamua kurejea kwenye nyumba ambayo alikuwa amepanga. Mwalimu Emmanuel aliamua kumusindikiza na kuingia naye chumbani,” alisema

“Mwanafunzi alimbembeleza mwalimu wake ambaye pia ni shemeji yake arudi kwake ili yeye aweze kujisomea, lakini mwalimu akikataa na kisha kumshika kwa nguvu na kumwingilia kimwili,” alisema Mkambala

Mwendesha mashitaka huyo alisema Januari 21, 2019 wazazi wa mwanafunzi huyo walimchukua binti yao na kwenda naye hadi kwa mkuu wa Shule kushitaki kwamba mtoto wao anakataa shule.

“Mwanafunzi huyo baada ya kuhojiwa alikiri kuwa ana mimba. Pia alitumia nafasi hiyo kutaja walimu waliomwingilia kimwili kuwa ni Ernest Emmanuel, Onesmo Bida, Keneth Komba na Ally Pangu. Walimbaka kila mmoja kwa muda wake,” alisema.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mkalmbala aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa washitakiwa na pia iongopeshe walimu wengine wanaotarajiwa kubaka wanafunzi.

Washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake walitoa maelezo yanayofanana kwamba bado ni vijana wadogo na wanategemewa kwa kiwango kikubwa na familia zao hivyo wapewe adhabu nafuu.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Makwaya alisema kitendo walichofanya walimu hao ambao wamepwa jukumu la kuwatunza na kuwalinda wanafunzi waweze kufikia malengo yao hakivumiliki.

“Wazazi wa mwanafunzi huyu waliwekeza kumwendeleza mtoto wao amalize masomo yake vizuri na kuwa na elimu ambayo ingesaidia wazazi hao kumaliza safari yao hapa dunia, vizuri.”

“Lakini ndoto hiyo imepotezwa na walimu kwa makusudi. Kwa kosa lenu la ubakaji, nafungwa mikono kulegeza hukumu, hivyo mtaenda jela kila mmoja miaka 30,” alisema

Chanzo: mwananchi.co.tz