Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu wanaotuhumiwa kuua mwanafunzi wafikishwa kortini

15269 Pic+walimu TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Jeshi la Polisi mkoani Kagera, limewafikisha mahakamani walimu wawili wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba wanaotuhumiwa kumuua kwa viboko mwanafunzi wa darasa la tano, Sperius Eradius (13) wa shule hiyo.

Walimu hao waliofikishwa mahakama ya wilaya ya Bukoba kusomewa mashtaka yanayowakabili leo asubuhi Septemba 3, 2018 ni Respicius Patrick Mtazangira anayetuhumiwa kumuua mwanafunzi huyo na Julieth Gerald.

Kesi hiyo imeibua hisia tofauti kwa baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye eneo la mahakama huku mtuhumiwa wa kwanza Respicius Mtazangira akionekana kuangua kilio huku akiwa na chupa ya maji mkononi.

Baadhi ya ndugu na marafiki wa mtuhumiwa wa pili Julieth Gerald baada ya kuteremka kwenye gari la Polisi walionekana kumfariji huku wakimfunika kwa vitenge asionekane sura yake.

Taarifa zaidi zinafuata.

Chanzo: mwananchi.co.tz