Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu wanane mbaroni kwa kuiba mtihani wa darasa la saba

15941 Walimu+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Buchosa. Watu wanane wakiwamo walimu wanne wa shule ya msingi Bulyahilu katika Kata ya Ilingamba Halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema, Mwanza wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa mitihani ya darasa la saba inayoendelea.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bahebe Kidesheni, wasimamizi watatu wa mitihani pamoja na mgambo aliyekuwa akilinda usalama wakati wa mitihani shuleni hapo jana Septemba 6.

Akizungumza na MCL Digital leo Septemba 6, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amethibitisha kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao na kwamba uchunguzi unaendelea kubaini namna walivyojihusisha wizi wa mtihani wa somo la Kiswahili.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa walimu hao waliuiba mtihani wa Kiswahili na kwenda kujifungia mahali kisha kuufanya kwa ajili ya kuwapa wanafunzi majibu.

Habari zaidi fuatilia mitandao ya MCL.

Chanzo: mwananchi.co.tz