Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu mbaroni kwa wizi wa Milion 200 Benki

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza, Wilboard  Mutafungwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilboard Mutafungwa

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Walimu 8 mkoani Mwanza wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma ya kuiba fedha zaidi ya Milioni 200 Kwa njia ya mtandao katika benki ya Akiba ya Waalimu iliyopo Jijini Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilboard Mutafungwa alisema,mnamo Februari 20 mwaka huu majira ya saa 9:21: Alasiri walipokea taarifa ya wizi huo kutoka kwenye uongozi wa Benki hiyo.

Aidha Mutafungwa alisema baada ya kufanya uchunguzi walifanikiwa kuwakamata Waalimu hao wakiwa na vitu mbali mbali ikiwemo fedha kiasi cha Milioni 20, pamoja na pikipiki mpya tatu zenye thamani ya Milioni 9 walizonunua kupitia fedha hizo.

"Waalimu hao wote ni wakazi wa Mkoa wa Mwanza waliiba fedha kiasi cha Milioni 273,800,000,katika Benki ya Akiba ya walimu kwa njia ya kuungilia mawasiliano na akaunti za benki kisha kuzihamishia pesa hizo katika akaunti zao ambazo ziko kwenye benki hiyo hiyo,"alisema Mutafungwa.

Aidha Mutafungwa aliwataja walimu hao ni Gasper Maganga mwalimu wa shule ya Msingi Kilabela, Marwa Samwel mwalimu wa shule ya Msingi Nyitundu, Aron Benard Mwalimu wa shule ya Msingi Bugumbikiso, Masaba Kiula mwalimu wa shule ya sekondari Kilabela,Cleva Gibson mwalimu wa shule ya sekondari Nyamatongo, Justne Otieno mwalimu wa shule ya Msingi Ishishangolo,wote ni wakazi wa Sengerema, Fredrick Awour mwalimu wa shule ya Msingi Pamba C Mkazi wa Ilemela na Stephen Sambali mwalimu wa shule ya Msingi Nyamgongwa Mkazi wa Nyang'wale mkoani Geita.

Watuhumiwa hao Bado wanahojiwa uchunguzi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live