Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walalamikaji kesi ya ‘Papa Msofe’ waja na hoja mpya

008967a6142805cfc164db227e3ac631 Walalamikaji kesi ya ‘Papa Msofe’ waja na hoja mpya

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WALALAMIKAJI katika kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, inayomkabili mfanyabiashara Marijan Msofe maarufu ‘ Papa Msofe’ na wenzake wanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wamedaiwa kuonesha nia ya kutokuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Hayo yalibainishwa jana na mmoja wa washtakiwa hao, Wenceslaus Mtui ambaye alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa akiwa gerezani alipokea barua kutoka kwa walalamikaji, iliyomuarifu kutokuwa na na nia ya kuendelea na mshtaka dhidi yao.

Mtui alizungumza kwa niaba ya washtakiwa wengine na kudai alipokea barua hiyo Oktoba 1, mwaka huu na kuongeza kuwa nakala za barua hiyo zipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na ofisi ya DCI, hivyo waliomba mahakama iwatajie tarehe za karibuni ili kufahamu suala hilo limeishia wapi.

Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka alidai mahakamani hapo kuwa hakuwa na taarifa kuhusu barua hiyo na kwamba haipo katika faili lake, hivyo alishauri ndugu wa washitakiwa, kufuatilia suala hiyo katika ofisi ya DPP.

Hakimu Shahidi alisema barua hiyo ilimfikia mezani kwake na alishauri ndugu wa washitakiwa, wafuatilie suala hilo katika ofisi za DPP.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi hadi Desemba 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Josephine Haule, Mwesigwa Muhingo na Fadhil Mganga.

Chanzo: habarileo.co.tz