Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakufunzi 4, wanafunzi 59 mbaroni kwa udanganyifu

C077236e3e6dffde472c410eca20d446 Wakufunzi 4, wanafunzi 59 mbaroni kwa udanganyifu

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inawashikilia wanafunzi 59 wa vyuo vya ufundi vya VETA na Tuinuane Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wakufunzi wanne na wakuu wa vyuo hivyo wawili kwa makosa ya udanganyifu wa mitihani ambapo walikuwa wakitumia simu za mkononi kufanya udanganyifu huo.

Kati ya wanafunzi hao, 38 wa VETA na wakufunzi wao ni Francis Mwangosi na Ssenabuly Daud pamoja na Mkuu wa chuo hicho, Baluhi Mitinje.

Wanafunzi 21 ni wa Chuo cha Tuinuane VTC kilichopo Karabagaine Halmashauri ya Bukoba pamoja na wakufunzi wao wawili ambao ni Chalse Byabachwezi, Verdiana Myaka na Mkuu wa chuo hicho, Emmanuel Jonas pamoja wasimamizi wawili ambao ni waajiriwa wa Chuo cha VETA Kagera walikamatwa kwa udanganyifu wa mitihani.

Mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Josephu alisema wanafunzi hao wamekamatwa katika operesheni maalumu baada ya kupata na taarifa ya kuwepo kwa udanganganyifu katika mitihani ya taifa ya elimu ya ufundi ambapo vyuo mbalimbali mkoani Kagera vimeanza mitihani ya taifa Desemba 7 mwaka huu.

Wanafunzi waliokamatwa katika mtihani huo walikuwa na simu 38 ambazo zilitumika kuwarushia wakufunzi wao maswali waliyoyakuta katika mtihani na wakufunzi hao walijibu maswali hayo kupitia simu zao.

Akizungumzia waliokamatwa kwenye chuo cha Tuinuane, alisema "Wanafunzi wa chuo cha Tuinuane waliingia na simu zao za kupiga maswali picha na kuwatumia wakufunzi wao kwa njia ya whatsApp ambapo wakufunzi walijibu maswali na kuyatuma kwa njia hiyo ya WhatsApp na ujumbe mfupi.

Chanzo: habarileo.co.tz