Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili wa utetezi kesi ya ghorofa augua kesi yashindwa kuendelea

Kesi Goirofaaaaaaaaa Wakili wa utetezi kesi ya ghorofa augua kesi yashindwa kuendelea

Thu, 19 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, imeshindwa kuendelea kusikiliza utetezi katika kesi kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo inayomkabili Mtunza fedha wa Kampuni ya World Wide Movers, Tuwaha Muze (44) na baba yake mzazi, Samson Tuwaha (71).

Baba na mwana huyo, wanakabiliwa na mawili likiwemo la kughushi mwenendo wa kesi ya ndoa na kughushi makubaliano ya uongo ya upangaji wa nyumba ya ghorofa moja iliyopo Mbezi Luis.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Adolf Verandumi ameieleza Mahakama hiyo hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, kuwa kesi hiyo namba 186/2019, imeitwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa utetezi kuendelea kutoa ushahidi.

Verandumi baada ya kueleza hayo, mshtakiwa kwa kwanza katika kesi hiyo, Tuwaha Muze alinyoosha mkono juu na alipopewa nafasi na mahakama ya kuongea, amedai kuwa amepewa taarifa na wakili wake, aitwaye Alexander Mzikila kuwa ni mgonjwa.

Muze amedai kuwa wakili wake amemuarifu kuwa anaumwa kifua na mafua na hivyo ameshindwa kufika mahakamani kuendelea na shauri hilo.

Muze baada ya kueleza hayo, Hakimu Mbuya amesema huo sio utaratibu wa kuwasilisha taarifa mahakamani, wakili Mzikila alipaswa aandikie barua Mahakamani au utume ujumbe mfupi kwenye simu ya mahakama ambayo ipo Maalumu kwa ajili ya kupokea ujumbe, ambao Mahakama ingeuona na sio kuwatuma washtakiwa kuja kutoa taarifa.

Advertisement Hakimu Mbuya baada ya kueleza hayo, ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 30, 2022 itakapoendelea na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Tayari Muze na baba yake ambao ni mashahidi wa upande wa utetezi wameshatoka ushahidi wao kuhusiana na mashtaka yanayowakabili.

Washtakiwa hao wanajitetea, baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kati ya Novemba 2011 na Desemba 2017 katika maeneo yasiyojulikana jiji Dar es Salaam, Muze na Samson kwa njia ya udanganyifu walighushi makubaliano ya uongo ya Novemba 9, 2011 kwa lengo la kuonyesha kuwa Samson ni mmiliki halali wa nyumba ya ghorofa moja iliyoko Mbezi Luis, huku mwanae aitwaye Tuwaha Muze ni mpangaji wa muda katika nyumba hiyo, wakati wakijua ni uongo.

Shtaka la pili, mwaka 2018, katika eneo la Kinondoni, mshitakiwa wa kwanza katika kesi hii (Tuwaha Muze), anadaiwa kuwa aliwasilisha nyaraka za uongo za mwenendo wa kesi ya ndoa namba 66/2017 katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akionyesha kuwa nyaraka hizo ni halali, wakati akijua kuwa nyaraka hizo ni za uongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live