Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili wa kujitegemea apandishwa kizimbani kwa kughushi

Nasra.jpeg Wakili Nasra Sangolo na Jumanne Mokili wakiwa ndani ya Mahakama ya H/M Kisutu

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili wa kujitegemea, Nasra Sangolo (32) anayeishi mkoani Mwanza na Jumanne Mokili (37) wa Isamilo Mwanza wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kughushi na kutoa nyaraka za uongo.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, Caroline Matemo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ritha Tarimo imedai kuwa Januari 16, 2021 katika mkoa wa Dar es Salaam , washtakiwa kwa nia ya kulaghai au kudanganya walighushi muhtasari wa kikao cha bodi cha kampuni ya Retrus Tanzania ltd.

Imedaiwa kuwa washtakiwa walighushi muhtasari huo kwa dhumuni la kuonesha kuwa umetolewa na kampuni hiyo ya Retrus huku wakijua kuwa siyo kweli.

Imeendelea kudaiwa kuwa, mwezi Julai mwaka 2021 huko katika ofisi za Brela zilizopo eneo la Lumumba jijinj Dar es Salaam, washtakiwa kwa makusudi kwa bia ya kulaghai walitoa nyaraka za kughushi za kikao cha bodi cha Retrus Tanzania Ltd kwa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakionesha kuwa ni za halali na zimetolewa katika kikao cha bodi cha kampuni hiyo ya Retrus huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wako huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wanaoishi Dar es Salaam watakaosaini bondi ya sh. Milioni mbili kila mmoja.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari Mosi, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live