Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili wa Sabaya ajitoa, atoa sababu hizi

8fd5249b7f5dea95cbb9bc89e4dc55e6.jpeg Wakili wa Sabaya ajitoa, atoa sababu hizi

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili wa Mshitakiwa wa tatu, Watson Mwahomange katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake sita ametangaza kujitoa.

Wakili Fridolini Bwemelo amebwaga manyanga baada ya kushindwa kuelewana na mteja wake namna ya kumlipa.

Akitangaza uamuzi huo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Bwemelo alimwambia Hakimu Patricia Kisinda kabla ya kuanza utetezi wa kesi hiyo kuwa hatakuwa tena akimwakilisha mshtakiwa katika kesi hiyo.

Upande wa utetezi umeanza kutoa utetezi wake na shahidi wa nne alikuwa mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo, Enock Mnkeni.

Hata hivyo waendasha mashtaka wa upande wa Jamhuri wamedai hawana pingamizi na uamuzi wa wakili. Vilevile, Mwahomange amedai kuwa yuko tayari kujisimamia katika kesi hiyo ambayo washtakiwa wengine ni John Aweyo, Sylivester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Sabaya na wenzake wawili tayari wanatumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia mwaka jana ya unyang’anyi wa kutumia slaha wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Watatu hao wamekata rufaa na shauri lao limepangwa kusikilizwa Machi 15 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live