Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili, hakimu wahoji upelelezi kesi ya bomba la mafuta kusuasua

32568 Mafutapic Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani (63) na wenzake 11 umeulalamikia  upande wa mashtaka kwa kuchelewesha upelelezi.

Wakili wa Serikali mwandamizi, Patrick Mwita amedai hayo leo Alhamisi Desemba 20, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa jalada hilo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),  wanaendelea kulifanyia kazi.

Mwita baada ya kueleza hayo, wakili wa utetezi, Alex Balomi amedai wimbo kuhusu upelelezi haujabadilika na washtakiwa wanaendelea kusota rumande.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote ameutaka upande wa mashtaka kuja na majibu ya kuridhisha kwa kuwa kesi hiyo imekaa muda mrefu.

“Hatutaki kuingilia mfumo wa upelelezi wenu. Hatutaki kuchelewesha shauri hili, wakati mwingine tutakapokutana hapa upande wa mashtaka mje na majibu ya kuridhisha vinginevyo sitawaelewa na sisi tunapata malalamiko mengi juu ya shauri hili,” amesema hakimu Simba.

Baada ya maelezo hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 3,2019.

Washtakiwa wote wapo rumande kutokana na DPP kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana.

Mbali na Nyakirang'ani, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nyangi Mataro (54) mwalimu wa Shule ya Msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Mfanyabaishara, Farijia Ahmed (39) mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias (39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus (25) mkazi wa Soko Maziwa, fundi ujenzi, Pamfili Nkoronko (40) mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail (43) mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.



Chanzo: mwananchi.co.tz