Dar es Salaam. Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa majadiliano kati ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP) na mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera bado unaendelea.
Katika kesi hiyo Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh173 milioni.
Leo Jumatatu Januari 27, 2020 Kabendera aliyekuwa amevaa suruali ya bluu na tisheti ya kijivu amefikishwa mahakamani hapo huku Mwenda akisema kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi haujakamilika.
Katika maelezo yake, Mwenda amesema majadiliano kati ya mshtakiwa na DPP bado yanaendelea, kuiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 10, 2020.
Kwa mara ya kwanza Kabendera alifikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019 akikabiliwa na makosa hayo anayodaiwa kuyafanya kati ya Januari 2015 na Julai 2019, jijini Dar es Salaam.
Habari zinazohusiana na hii
- VIDEO: Simanzi Kabendera afikishwa Mahakama ya Kisutu, afuta machozi
- VIDEO: Serikali ya Tanzania yampa pole Erick Kabendera kufiwa na mama yake, yapinga kwenda kumuaga
- VIDEO: Mahakama kutoa uamuzi Erick Kabendera kumuaga mama yake
- Mahakama yamzuia Erick Kabendera kwenda kumuaga mama yake
Shtaka la pili anadaiwa katika kipindi hicho bila ya sababu alikwepa kodi ya Sh173.2 milioni aliyotakiwa kulipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika shtaka la tatu, anadaiwa kutakatisha Sh173.2 milioni huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.