Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili anayetuhumiwa kusambaza picha za makonda aachiwa

Fd Makonda Wakili anayetuhumiwa kusambaza picha za makonda aachiwa

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jioni ya Aprili 30, 2024 Jeshi la Polisi lilimkamata Wakili Yonas Masiaya kwa tuhuma za kusambaza picha ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda katika makundi ya WhatsApp huku ikidaiwa Polisi walikataa kumpa dhamana licha ya Sheria kuruhusu

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) ulitoa tamko la kulaani tukio hilo huku ukielekeza Mawakili wake Mkoani Arusha kufuatilia kwa karibu suala hilo.

JamiiForums imewasiliana na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, kuhusiana na tukio hilo ambapo amesema "Tulitoa tamko la kulaani kama mlivyoona, na tuliwapa Vijana kazi ya kuandaa lakini wakati tupo kwenye mchakato muda si mrefu kama saa moja ameachiliwa kwa kupewa masharti kwamba kesho akaripoti"

Alipoulizwa kuhusu sababu ya kukamatwa amesema; "Ni picha, nadhani 'alishare' picha kwenye magrupu ya WhatsApp akionekana Mkuu wa Mkoa ameingia kwenye Hoteli fulani, nadhani kuna tuhuma zilikuwepo kwamba anakaa Hoteli fulani, sasa hiyo picha hawakupenda kuona inasambaa."

Wito umetolewa kwa Jeshi la Polisi:

Kumwachia wakili Masiaya kwa dhamana. Kufanya upelelezi kwa kuzingatia Sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO), bila kusubiri maelekezo kutoka juu ambayo ni nje ya utaratibu wa kisheria. Kufanya upelelezi kabla ya kumkamata wakili Masiaya endapo kuna tuhuma dhidi yake. Kudai mabadiliko ya sheria ya makosa ya kimtandao ili kulinda uhuru wa watanzania katika matumizi yao ya mitandao kwa kuzingatia Sheria za ulinzi wa taarifa na faragha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live