Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili akwamisha rufaa ya Serikali dhidi ya Nondo

66835 Pic+wakili

Mon, 15 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa imeahirisha kusikiliza rufaa ya Serikali dhidi ya aliyekua mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo kutokana na wakili anayemwakilisha Nondo kutofika mahakamani.

Serikali ya Tanzania ilikata rufaa katika Mahakama Kuu kupinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa iliyomwachia huru Nondo aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka mawili.

Mashtaka hayo ni kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwamba katika hali ya hatari akijua ni uongo  kinyume na sheria ya mtandao ya mwaka 2016  na shtaka la pili ni kulidanganya jeshi la polisi Mjini Mafinga kwamba alikuwa ametekwa akijua kwamba ni uongo na ni kinyume cha sheria.

Leo Jumatatu Julai 15, 2019, Wakili wa utetezi, Edrick Mwinuka ameiambia Mahakama kuwa wakili anayesimamia kesi hiyo Chance Luoga anaumwa na hajampatia  maelezo ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mwinuka ameieleza mahakamani wakili anayesimamia kesi hiyo amemuagiza kuahirisha.

Naye wakili wa Serikali, Abedi Mwandalamo anayewakilisha upande wa mkata rufaa amesema rufaa imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na wao wapo tayari.

Pia Soma

Hata hivyo, Jaji Panterine Kente anayesikiliza kesi hiyo ameahirisha hadi Septemba 4, 2019.

Miongoni kwa sababu iliyoifanya Jamhuri  kukata rufaa ni kupinga hakimu aliyetoa toa uamuzi wa kumwachia Nondo huru hakuzingatia masharti ya kifungu cha 214 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.

Chanzo: mwananchi.co.tz