Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili akwamisha kesi ya anayedaiwa kuisababishia TRA hasara ya Sh188bilioni

32553 Mashinepic Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dara es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Sh188.9bilioni  kupitia mashine ya risiti za kielekroniki (EFD)  inayomkabili  mfanyabiashara Mustapha Kambangwa (34), bado haujakamilika.

 

Kambangwa, mkazi wa Mbagala Kongowe anakabiliwa na mashtaka manne Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, likiwemo la  kutakatisha fedha katika.

 

Kwa mara ya kwanza, Kambangwa  alifikishwa mahakamani hapo Desemba 7, 2018  kujibu mashtaka manne  katika kesi ya uhujumu uchumi namba 19/ 2018.

 

Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai leo Alhamisi Desemba 20, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upande wa utetezi kuwasilisha hoja za kupinga shitaka dhidi ya mshtakiwa.

 

Hata hivyo,  hoja hizo hazikuwasilishwa mahakamani hapo baada ya Ester kudai  kwamba wakili mwenzake Christopher Msigwa, ambaye ndio mwenye jalada halisi la kesi hiyo ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa.

 

Baada ya upande wa mashtaka kueleza hayo, wakili wa utetezi Shamo Shadrack, amedai ofisi ya waendesha mashitaka ina  mawakili wengi na kuhoji sababu za  kuumwa kwa mtu mmoja kuzuie kesi kuendelea.

 

" Kuumwa kwa mtu mmoja kusizuie kuendelea kwa kesi, kwani mawakili wote wanafanya kazi ofisi moja hivyo tunaomba tarehe ijayo ambayo ni Desemba 24, 2018 tuweze kuwasilisha hoja zetu, " amedai Shadrack.

 

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Janeth aliwataka upande wa mashitaka kuhakikisha shauri hilo linaendelea hata kama yule wa  awali bado anaumwa aendeshe mwingine.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 24, 2018 na mshtakiwa kurejeshwa rumande.

 

Katika  kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hiyo kati ya Juni Mosi ,2016 na Novemba 2, 2018.

 

Katika shtaka la kwanza, Kambangwa alijifanya amesajiliwa  kuwa mlipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

 

Amedai katika tarehe tofauti kati ya Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, 2018 maeneo ya jiji la Dar es Salaam mshitakiwa alijifanya kuwa amesajiliwa kukusanya kodi ya VAT  Sh 188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya TRA.

 

 

Pia, Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, 2018, Kambangwa kwa udanganyifu alitumia mashine ya EFD namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham's Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani ya fedha hiyo

 

Katika shtaka la tatu, ambalo ni utakatishaji wa fedha, mshtakiwa anadaiwa, tarehe na kipindi hicho, katika Jiji la Dar es Salaam alijipatia au kujimilikisha fedha hizo alizozipata kutokana na makato ya kodi ya VAT ambazo zilipaswa kutolewa kwa Kamishna wa TRA na mshitakiwa huyo alipaswa kujua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la ukwepaji kodi

 

Kati ya Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, 2018 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa  kwa vitendo vya makusudi vya kukwepa kodi alitumia mashine ya EDF huku akijua kwamba hajasajiliwa kama mlipakodi ya VAT na hivyo kuisababishia hasara TRA  ya 188,928,752,166

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz