Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili akwamisha Kesi ya Jamii Forum

47457 Kesipic

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kesi ya kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwenzake Micke William, imeshindwa kuendelea kutokana na wakili wa Serikali anayeendesha kesi hiyo kutokuwepo.

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala amedai leo Jumanne Machi 19, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya utetezi lakini wakili anayesimamia kesi hiyo hayupo.

"Kesi imekuja kwa ajili ya utetezi, Wakili anayesimamia kesi hii hayupo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na shauri hili," amedai Wakili Makakala

Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai kutokana na wakili wa Serikali kutokuwepo hawana pingamizi kuhusiana na hoja hiyo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Aprili 18, 2019 kwa ajili ya washtakiwa kujitetea.

Tayari mashahidi wanne wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa hao na Mahakama kuwakuta na kesi ya kujibu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, kinyume na Sheria Namba 22 (2) ya Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Aprili Mosi, 2016 na Desemba 13, 2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni.

Soma Zaidi: Uamuzi kesi ya Jamii Forum kutolewa Februari 22



Chanzo: mwananchi.co.tz