Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili afungwa jela miaka 7 kwa kumuua mpenzi wake

Kortinipic Data Wakili afungwa jela miaka 7 kwa kumuua mpenzi wake

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili wa kujitegemea, Steven Mduma amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kumkuta na hatia ya kumuua mpenzi wake Jackline Mwanjombe bila kukusudia.

Jackline aliuawa Oktoba 4,2020 huko Kimara Bucha nyumbani kwa mshtakiwa baada kulewa pamoja katika baa tofauti tofauti.

Hukumu hiyo imesomwa mwishoni mwa wiki na Jaji Nkwabi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Nkwabi amesema amemtia hatiani baada ya kuridhika na ushahidi wa shtakiwa mashahidi saba na kielelezo kimoja ambacho ni taarifa ya uchunguzi wa kifo uliotolewa na upande wa Jamhuri.

"Kesi hii imeangalia zaidi ushahidi wa kimazingira mtu wa mwisho kuwa na marehemu alikuwa ni mshtakiwa na pia taarifa ya uchunguzi wa Dkt. inanishawishi kuwa marehemu hakufa kifo cha kawaida (natural death) na pia mshtakiwa kwa kuwa yeye ndio alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu alipaswa kueleza ni kitu gani kulisababisha kifo cha marehemu" amesema Jaji Nkwabi

Ameongeza kuwa kukinzana kwa ushahidi wa mashahidi wa utetezi unamuweka mshtakiwa kwenye nafasi ya kumtilia shaka kwani mashahidi wake wote walitoa ushahidi ambao ulikuwa utatofautiana.

"Mshtakiwa katika utetezi wake alidai kuwa marehemu alikuwa amelewa sana akaishiwa nguvu na kufariki lakini Dkt. Praxeda Ogweyo alipofika mahakamani hapa kutoa ushahidi wake alidai uchunguzi wa kifo cha marehemu (Postmortem Report) ulionyesha kuwa marehemu alikufa kwa kukosa hewa iliyosababishwa na kugandamizwa na kitu nje ya shingo(external false).

Pia ripoti hiyo inaonyesha mfupa wa shingo wa mshtakiwa ulivunjika na pia mapafu yake alikaa maji na sehemu zingine zilionekana kuvilia damu.

Baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani, Jaji Nkwabi aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili wa serikali Judith Kiamba akisaidiana na wakili Grace Mwanga wakaiomba mahakama mshtakiw apewe adhabu kali.

"Mheshimiwa pamoja na kwamba mshtakiwa ni mmkosaji wa kwanza lakini kuna uhai wa mtu umetoka, tunaomba apewe adhabu kali iwe Faraja kwa wafiwa", amesema Judith.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live