Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Takukuru akwamisha kesi ya vigogo Rahco

50106 KESI+PIC

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kueendelea na kesi  ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco) baada ya wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo anayeendesha shauri hilo kupata udhuru.

Vigogo hao katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito, mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patric Mwita ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo  ilikuja kwa ajili kuitolea maamuzi madogo hivyo wakili anayeendesha shauri hilo Ndimbo amepata udhuru.

"Wakili Ndimbo amepata udhuru ameiomba mahakama hii ipange tarehe fupi kama itawezekana kesho au keshokutwa atakuwepo," alidai Mwita.

Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba alisema upande wa Serikali anayesikiliza shauri hilo hayupo na upande wa utetezi wote hawapo, ni vizuri wote wakiwepo wakati maamuzi madogo ya shauri hilo yakitolewa.

Simba aliahirisha shauri hilo hadi keshokutwa, Aprili 4, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kuitolea maamuzi madogo na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shauri hilo kutokuwa na dhamana.

Februari 27,2019, wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alitoa hoja na kudai kuwa kesi za uhujumu uchumi zinasikilizwa na Mahakama Kuu na kutaka upande wa utetezi kupewa nakala za nyaraka za mashahidi pamoja na vielelezo vyote.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 kwa nia ya kutenda kosa walikula njama kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Ilidaiwa kuwa Februari 27, 2015 katika ofisi za Rahco zilizopo Ilala, Tito alitumia madaraka yake vibaya kwa kuiajiri Kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Ltd kama mshauri wa mradi wa uimarishaji reli ya kati bila idhini ya Bodi ya Zabuni ya Rahaco.

Ilidaiwa kuwa Tito na Massawe, Machi 12, 2015 katika ofisi za Rahco Ilala wakiwa katika nyadhifa zao, walisaini barua ya kuihalalisha kampuni hiyo ya Afrika Kusini kuwa mshauri wa mradi wa uimarishaji reli ya kati na kutoa huduma za ushauri wa kifedha kuhusu mradi huo.

Katika shtaka jingine, ilidaiwa kuwa Tito na Massawe, Machi 12 na Mei 20, 2015 wilayani Ilala walishindwa kuwasilisha mkataba wa huduma ya ushauri kati ya kampuni hiyo ya Afrika Kusini na Rahco.

Soma zaidi>> Vigogo Rahco wafikishwa kortini

Tito na Massawe wanadaiwa Mei 20, 2015 katika ofisi za Rahco, kwa kutumia madaraka yao vibaya walisaini mkataba wa kutoa huduma za ushauri na kampuni ya Afrika Kusini bila ridhaa ya Bodi ya Zabuni ya Rahco.

Washtakiwa hao, wanadaiwa kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015 walitumia madaraka yao vibaya kwa kushindwa kuwasilisha mkataba walioingia na kampuni ya Afrika Kusini kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Tito, Mwinyijuma na Massawe, wanaodaiwa kati ya Machi Mosi na Septemba 30, 2015 katika ofisi za Rahco, waliipa kazi kampuni hiyo ya ushauri na kuilipa kwa kutoa huduma za ushauri, malipo yaliyosababisha Rahaco kupata hasara ya Dola 527,540.

Ilidaiwa kuwa Agosti 18, 2015 katika ofisi za Rahco Ilala, Tito alitumia madaraka yake vibaya, aliipa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China kazi ya kujenga kilomita mbili za reli maeneo ya Soga iliyogharimu Dola 2,312,229.39 bila idhini ya Bodi ya Zabuni ya Rahaco.

 Soma hapa>> Mahakama yaombwa kufuta kesi ya vigogo Rahco

>>Hakimu ashindwa kutoa uamuzi kesi ya vigogo Rahco

>> Mahakama yaomba siku mbili kupitia jalada vigogo Rahco



Chanzo: mwananchi.co.tz