Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Mwale ahukumiwa kulipa faini Sh200 milioni au kifungo cha miaka mitano

29928 Mwale+pic TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Jaji Issa Maige wa Mahakama Kuu Arusha leo Jumatatu Desemba 3, 2018 amemhukumu wakili Medium Mwale kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh200 milioni kutokana na kosa la utakatishaji fedha.

Pia amemuhukumu kifungo cha miaka saba ambacho ameshakitumikia kutokana na makosa mengine.

Katika kesi hiyo wakili Mwale na wenzake, Boniface Mwimbwa aliyekuwa meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru na Elias Ndejembi wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo kughushi na utakatishaji fedha.

Katika kesi hiyo, aliyekuwa mshitakiwa wa pili, Donbosco Gichana (raia wa Kenya) alikiri makosa ya kula njama na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani  5,296,327.25 na kuamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo gerezani.

Gichana alilipa faini hiyo na tayari aliondoka nchini kurejea Kenya.

Soma zaidi:

Rufaa ya Wakili Mwale na wenzake yagonga ukuta

Wakili azidiwa mahakamani, kesi yaahirishwa

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz