Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Msando mbaroni kwa madai ya kuzua hofu juu ya corona

POLISI.webp Wakili Msando mbaroni kwa madai ya kuzua hofu juu ya corona

Thu, 30 Apr 2020 Chanzo: --

Kamanda Moita ameyabainisha hayo leo Aprili 30, 2020, na kusema kuwa Msando alieleza kuwa hali mbaya ya ugonjwa wa corona ndani ya Mkoa wa Arusha kupitia video yake iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akizungumza na waandishi wa habari baada ya kugawa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizo ya corona.

"Hali hii ilitoa wakati mgumu kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza, kauli hii aliitoa wakati anatoa vifaa vya kujikinga na corona katika eneo la Kaloleni katika Ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, na Serikali ilikwishatoa maelekezo kuwa mwenye mamlaka ya kutoa tarifa hizo ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu, hii kauli lazima iheshimiwe" amesema Kamanda Moita.

Kauli ya Msando : "Ukweli ni kwamba na niseme bila kuficha hali ni mbaya kwa Arusha na ndugu waandishi nyinyi ni lazima mfike mahali muweke miguu chini mseme ukweli ili wananchi, Serikali na kila anayehusika atambue kwamba tupo katika hali mbaya, ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua mkirudi nyuma na kuogopa kusema tutazikana.," Kaimu Kamanda Moita alinukuu Maneno anayodai kuyasema Msando

Amesema Polisi wamechukua hatua hiyo kutokana na Msando kukiuka maelekezo ya Serikali kuwa wenye Mamlaka ya kutoa taarifa za ugonjwa huu ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu wa Serikali.

Sambamba na hilo Polisi mkoani humo inamshikilia Agness Shinji mkazi wa Lemara kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo mitandaoni.

Kaimu Kamanda Moita amesema Aprili 9,2020 Agness Shinji akitumia Kundi Songezi 'WhatsApp Group' liitwalo "Football fo life" alituma taarifa kuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC1 Gloria Maiko amefariki Dunia kutokana na ugonjwa wa corona jambo ambalo si kweli na kusabisha taharuki kwa ndugu jamaa na marafiki.

Amesema baada ya polisi kubaini kuwa ni uzushi lilianza kumfuatilia Agness na Aprili 29,2020 alikamatwa ambapo alikiri kutuma ujumbe huo wa kifo cha mtangazaji huyo bila ya kuwa na uhakika.

Kamanda Moita, amesema watuhumiwa wote wawili watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo: --