Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Afunguka Ugonjwa Unaomsumbua Sabaya

Video Sabaya Pic Data Wakili Afunguka Ugonjwa Unaomsumbua Sabaya

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

WAKILI namba mbili wa Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya, Faudhia Mustapha ameieleza mahakama kuwa, jana jioni alienda kumjulia hali Mteja wao katika Gereza kuu Arusha Kisongo na kuzungumza naye pamoja na daktari anayemtibu na kuelezwa kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa wa vidonda vya tumbo alivyovipata akiwa gerezani na anasumbuliwa na uti wa mgongo tatizo alilolipata kabla ya kwenda gererezani.

Leo Novemba 4, 2021 kesi namba 27/2021 ya uhujumu uchumi inayomkabili Lengai Ole Saba ya na wenzake sita ilitakiwa iendelee kusikilizwa lakini imeahirishwa baada ya upande wa jamhuri kupinga kesi hiyo kuendelea bila uwepo wa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Lenagi Sabaya.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Novemba 5, 2021 ambapo mahaka imetaka mawakili wa utetezi kuja na barua ama ruhusa ya maandishi ya Lengai ole Sabaya kuwaruhusu waendelee na kesi hiyo kusikilizwa bila uwepo wake.

Chanzo: globalpublishers.co.tz