Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakenya wanaswa Tanzania na magunia 15 ya mirungi

Mirungi Chuga.jpeg Wakenya wanaswa na mirungi

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAFANYABIASHARA wawili wa Kenya, wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha wakituhumiwa kuwa na magunia 15 ya mirungi.

Wakenya hao wanatuhumiwa kumiliki mirungi hiyo na kuisafirisha kwenda maeneo mbalimbali Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kukamatwa kwa wafanyabiashara hao na kusema bado uchunguzi wa tukio hilo haujakamilika, lakini ukishakamkilika jalada litafikishwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa hatua nyingine.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Namanga, wakiwa katika gari ndogo aina ya Toyota Forester yenye namba za usajili KDC 922T, iliyokuwa ikiongoza gari kubwa, lililokuwa limebeba shehena hiyo Mei 14, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live