Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi wa Dar wawekwa chini ya uangalizi kwa kukutwa na dawa za kulevya

Wakazi Wa Dar Chini Ya Uangalizi Wakazi wa Dar wawekwa chini ya uangalizi kwa kukutwa na dawa za kulevya

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaweka chini ya uangalizi watu watatu wakazi wa Dar es Salaam kwa kudaiwa kukutwa na dawa za kulevya.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Ramadhani Juma, Musa Ramadhani na Doto Masanja.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo leo baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili wa serikali Monica Ndakidemi kuiomba mahakama hiyo kufanya hivyo baada ya kupata taarifa za awali zinazoonesha kwamba watu hao wanajihusisha na dawa za kulevya ambazo hazikubainishwa.

Akitoa maelezo baada ya mahakama kutoa ombi hilo Hakimu Mkazi Evodia Kyaruzi ameeleza kuwa uangalizi unajumuisha kila mmoja wao kuwaleta wadhamini wawili ambao watahakikisha wanakuwa na tabia njema kwa muda wa miaka mitatu.

Agizo lingine lililotolewa na mahakama hiyo ni kuwataka watuhumiwa wote kuripoti katika ofisi za Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kila mwisho wa mwezi.

Pia, mahakama imewaagiza kutojihusisha na matendo yoyote ya kihalifu kwani kufanya hivyo kutawafanya wafunguliwe mashitaka.

Aidha, watuhumiwa hao walipoulizwa kama wana lolote la kusema kuhusu maagizo hayo walisema wamekubaliana na maagizo hayo na watayatekeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live