Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakatwa vidole na vijana wawili waliotaka kuwabaka

Mikono Kata Wakatwa vidole na vijana wawili waliotaka kuwabaka

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wawili katika Kijiji cha Malangi kata ya maisaka mjini Babati Mkoani Manyara wamejeruhiwa na kitu chenye ncha kali mara Baada ya kunusurika kubakwa huku Mmoja Kati yao aking'atwa shavu na kijana aliyefahamika kwa jina la Ally Jacobo alimaharufu (Nyeusi Ngumu)Mkazi wa kijiji hicho.

Wakizungumza viongozi wa Kijiji hicho akiwemo mwanyekiti na Mtendaji wamekiri kutokea kwa matukio hayo siku ya Alhamisi iliyopita, huku mtuhumiwa akitokomea kusiko julikana na juhudi za kumsaka Zinaendelea.

Kwa upande wao manusura wa matukio hayo akiwema mama aliye jeruhiwa vidole na kung'atwa shavu amesema mtuhumiwa Ally Jacobo alimvamia Nyumbani kwake majira ya saa 10 jioni nakuanza kufanya tukio hilo ndipo alipo pambananaye na kupiga kelele na mtuhumiwa kumjeruhi na kung'atwa shavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live