Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamwatwa wakisafirisha bangi gunia 10

1198 BANGIII 660x400 Wakamwatwa wakisafirisha bangi gunia 10

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu watano pamoja na magari manne wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya magunia kumi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amesema hayo leo kwa waandishi wa habari, kuwa June 7, majira ya usiku maeneo ya Kibaha walimkamata Said Mohamed (43) mkazi wa Kipunguni B, jijini Dar es Salam, akisafirisha bangi gunia kumi kwa kutumia gari lenye namba za usajili T852 AYV aina ya Toyota akitokea Mikumi kuelekea Dar es Salaam.

Amewataja waliokamatwa ni Jeremia Samwel (29) na Faizia Kindamba (26) wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam wa waliokamatwa eno la Ubena Chalinze wakisafirisha bangi iliyokadiriwa kuwa kilogramu 55 zikiwa zimefungwa kwenye mabegi makubwa manne na dogo moja wakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 809 DKQ aina ya Noah.

Amesema mtuhumiwa Alex Mkiri (43) alikamatiwa eneo la Bwawani Chalinze akisafirisha bhangi viroba vitano kwenye gari namba T 332 DLE aina ya Toyota IST kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam, na huko Picha ya Ndege Wilaya ya Kibaha.

Amesema jeshi hilo lilikamatwa bajaji yenye namba za usajili TMC 484 AJJ, ikiwa na viroba viwili vikiwa na bhangi kilo 26, mtuhumiwa alitoroka kabla ya kukamatwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live