Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa wakisafirisha madumu 3,500 mafuta ya kula

FC2E91C7 BAD7 4A03 8C87 6E325C3DD890.jpeg Wakamatwa wakisafirisha madumu 3,500 mafuta ya kula

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi kikosi cha Wanamaji, linamshikilia nahodha Amme Maulid (37) mkazi wa Pemba na wenzake tisa wakiwa na jahazi kubwa aina ya Bumu liitwalo MV Yeshasemwa likiwa limebeba shehena ya mafuta ya kula madumu 3,500 yenye ujazo wa lita 20 kila moja.

Jahazi hilo lenye usajili wa namba Z 2025 lilikamatwa Novemba 24, mwaka huu katika kisiwa cha Kwale Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, likitokea Zanzibar kuelekea Lindi.

Taarifa iliyotolewa jana Jumamosi Novemba 26, 2022 na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji, Sokoro Moshi imeeleza kuwa, upelelezi wa awali umeonyesha mzigo huo hauna vibali vya kusafrishia kutoka mamlaka husika za Zanzibar.

“Jeshi la Polisi linashirikiana na TRA na idara nyingine za Serikali kuhakiki mzigo huo na baadae taratibu nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa,” amesema Kamanda Moshi.

Aidha Jeshi la Polisi linawapongeza wananchi wote wanaochukia uhalifu, na kutoa taarifa zanazowezesha kukamatwa kwa watu wote wanaojihusisha na uhalifu.

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa wafanyabiashara wasio na uadilifu, kufuata taratibu za TRA lasihivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi,” amesema.

Hivi karibuni Meneja Udhibiti na Ushurutishwaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Eekieli Gisunte amesema ukanda wa Pwanni bado kuna shida katika upitishaji wa bidhaa za magendo kupitia Bahai ya Hindi.

Amesema vijana wengi wa maeneo hayo wamekuwa wakijipatia kipato kwa njia zisizohalali, jambo linalosababisha Serikali kukosa mapato au kuingiza bidhaa zisizo na ubora.

Chanzo: Mwananchi