Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa na swala 28 waliouawa

Swala Mssd Wakamatwa na swala 28 waliouawa

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wakazi wa kijiji cha Mwasilimbi kata ya Ihusu Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo, kwa tuhuma za kukutwa na Wanyamapori aina ya swala 28 wakiwa wamewaua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Edith Swebe akizungumza na waandishi wa Habari leo Ofisini kwake, amasema kuwa watu hao walikamatwa katika opereisheni ya pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Uhifadhi.

Swebe amewataja watu hao kuwa ni Masunga Madede (58), Musa Masunga (28) na Yunis Makwaya (45) wote wasukuma na wakazi wa kijiji hicho cha Mwasilimbi.

“Watuhumiwa hawa walikutwa na Nyara za serikali ambazo ni wanayamapori swala 28 aina ya Thomson wakiwa wameuawa, Swala hao walikuwa wamepatikiwa kwenye Pikipiki aina ya KingLion nyekundu iliyosajiliwa kwa namba T.874 CUA” Amesema Kamanda Swebe.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa watuhumiwa pamoja na vielelezo watafikishwa mahakani kwa hatua za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live