Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa na meno ya Tembo

Meno Ya Tembopicc Wakamatwa na meno ya Tembo

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: mwananchidigital

eshi la Polisi Mkoani Tanga limekamata meno mawili ya tembo na moja la kiboko yenye thamani ya Sh37.9 milioni

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani hapo, Safia Jongo amesema jeshi hilo pia limekamata vipande 20 vya swala vyenye uzito wa kilo40 vyenye thamani ya Sh1.5milioni.

Kamanda Jongo amesema jeshi hilo linawashikilia wanaume wawili waliokamatwa na nyara hizo walizokuwa wamezihifadhi katika mfuko.

Vile vile, Kamanda Jongo ametoa onyo kwa wakazi wa mkoa huo wanaosambaza taarifa za uzushi juu ya mwanamke kukatwa tumbo na watoto wa ‘Ibirisi’.

Amesema jeshi hilo limewafikisha mahakamani watoto wa ‘Ibirisi’ 130 kwa hatua zaidi za kisheria.

Vile vile, Kamanda wa Polisi amesema wamewakamata watuhumiwa nane kwa madai ya kuiba Air condition 10 pamoja na gari aina ya Suzuki iliyotumika kubeba mali hiyo.

Chanzo: mwananchidigital