Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa kwa kuua Pundamilia na Digidigi

PUNGGAA Wakamatwa kwa kuua Pundamilia na Digidigi

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia wakazi wanne wa wilayani Mwanga kwa tuhuma za kufanya ujangili ambapo wanadaiwa kuwauwa kwa kuwapiga risasi na kuwacharanga mapanga Pundamilia watatu na digidigi mmoja.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuhujumu uhai wa wanyama hao katika  pori la Karabandea linalopakana na hifadhi za Taifa za Mkoamazi mkoani Kilimanjaro na Tsavo inayoambaamba Kusini Mashariki mwa Nchi jirani ya Kenya.

Mamlaka za serikali katika wilaya ya Mwanga zikiongozwa na mkuu wa wilaya Abdallah Mwaipaya ndizo zilizoanza harakati za kufuatia nyendo za watuhumiwa hao baada ya kupewa taarifa na wananchi.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Kamishina Msaidizi wa Polisi Simon Maigwa, amesema watu hao walitumia kuwauwa wanyamapori hao kwa kutumia bunduki na ambayo bado haijakamatwa .

   

Chanzo: Eatv