Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa kwa kosa la kuficha magunia 26 ya bangi kanisani

Bangi Pic Wakamatwa kwa kosa la kuficha magunia 26 ya bangi kanisani

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanaume wawili wamekamatwa na jeshi la Polisi nchini Kenya kwa kosa la kuficha magunia 26 ya dawa za kulevya aina ya bangi ndani ya kanisa.

Tovuti ya Taifa Leo ya nchini humo imesema mbali na magunia hayo ya bangi watuhumiwa pia wamekutwa na nyama ya mbuzi pamoja na vifaa vya kielektroniki.

Taarifa zinasema vitu vyote hivyo vimekutwa katika kanisa la African B lililoko eneo la Ongata Rongai, kaunti ndogo ya Kajiado Kaskazini inayopakana na Nairobi na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro iliyopo Tanzania.

Jana Jumatatu raia wenye hasira walipata fununu kuwa vitu hivyo vilikuwa katika kanisa hilo ambapo walienda na kuwakuta wakitayarisha nyama hiyo ya mbuzi.

Inaelezwa kulitokea vurumai baina ya raia na watuhumiwa hao pamoja na watu waliokuwepo kanisani. Polisi walifika eneo hilo na kuzuia sekeseke hilo ambalo lilipelekea jaribio la kubomolewa kwa kanisa.

Naibu Kamishna wa Kajiado Kaskazini, James Taari, ameasema walipofanya msako ndani ya kanisa hilo, walipata magunia 26 ya bangi na vifaa hivyo vya kielektroniki.

Kwa sasa watuhumiwa wanashikiliwa kituo cha polisi cha Ongata Rongai kabla ya kufikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live