Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakala wa benki akwapua fedha za mteja, ahukumiwa jela

FEDHA WEB Wakala wa benki akwapua fedha za mteja, ahukumiwa jela

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Wakala wa fedha kupitia benki ya NMB tawi la Lindi mjini, Abdulrahamani Ally Madulu, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezano, baada ya kukutwa na kosa la  wizi wa jumla ya shilingi milioni 2 kwa mteja wake, Fatuma Ally Nassoro.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Lindi mjini, Hamisi Kafumba, baada ya kuridhishwa pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji.

Baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia, Hakimu alimuuliza iwapo ana jambo la kuiambia Mahakama ili isimpe adhabu kali kwa kosa linalomkabili, akijitetea mshtakiwa Madulu akaomba apewe nafuu ya adhabu, kwani ana familia inayomtegemea, wakiwemo watoto wadogo, mke, wazazi na wajukuu.

Hakimu Kafumba akitoa hukumu kesi ya wizi Namba 125/2022 kupitia kifungu 258 na 265 kanuni ya adhabu sura ya 16,rejeo la mwaka 2022, alisema kutokana na uzito wa kosa, shufaa na shufaa alizonazo, Mahakama inampa adhabu ya kulipa faini ya Sh,200,000/-na akishindwa atumikie kifungo cha miezi mitatu gerezani.

Pia,Mahakama hiyo imemuamuru mshtakiwa Maduhu kurejesha kwa mlalamikaji Fatuma Ally Nassoro,shilingi milioni 2 alizobaki nazo mara baada ya kumaliza kutumikia adhabu au baada ya kulipa faini aliyopewa.

Mshitakiwa amebahatika kulipa faini na kunusulika kwenda kutumikia kifungo na kubaki kurejesha fedha alizoiba kutoka kwa mlalamikaji, Fatu Ally Nassoro.

Awali ilidaiwa Mahakamani hapo Septemba 04 mwaka huu, saa 9:00 alasiri, mlalamikaji Fatuma Ally Nassoro alikwenda kwa wakala huyo, Abdurahmani Ally Madulu, na kumpatia shilingi milioni 4, kwa lengo la kumuwekea katika akaunti yake iliyopo Benki ya NMB tawi la Lindi mjini na badala yake alimuingizia kiasi cha shilingi milioni 2 pekee.

Chanzo: Eatv