Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajiandaa kufikisha kortini ‘waliokwapua’ AUWSA

3e2df4cccb8260ca79d67911aa3513cd Wajiandaa kufikisha kortini ‘waliokwapua’ AUWSA

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), John Mbungo amesema wapo katika hatua ya mwisho ya uchunguzi wa ubadhirifu,ukiukwaji wa sheria na taratibu za ununuzi katika ujenzi wa ofi si za Kanda ya Mamlaka ya maji Jijini Arusha (AUWSA) .

Alisema hayo jijini Arusha na kusema mradi huo una thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.3 na kwamba uchunguzi umethibitisha uwepo wa ukikwaji wa taratibu za manunuzi hivyo taratibu za kisheria zinaandaliwa na wahusika watafikishwa mahakama.

‘’Uchunguzi wa awali wa Takukuru umebaini ukikwaji wa taratibu za manunuzi hivyo taratibu za kisheria zinaandaliwa na wahusika watafikishwa mahakamani wakati wowote’’alisema Mbungo.

Alisisitiza kuwa Takukuru haitakuwa na msalimie mtume kwa watendaji wa serikali na taasisi zake wanaokiuka taratibu za manunuzi kwa maslahi yao.

Alisema Rais John Magufuli amewaagiza wao kuhakikisha haki na matumizi ya rasilimali za umma zinatumika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila mmoja anafuata taratibu zilizowekwa na serikali. Wakati huo huo alisema kero ya pili iliyochunguzwa na Takukuru ni pamoja na mgogoro uliowahusisha wakulima 83 waliokuwa kwenye eneo la mashamba ya Malula kwa upande mmoja na Safia Okash kwa upande .

Walikuwa wakigombea umiliki wa eneo lenye ukubwa wa ekari 2,456 lililopo katika shamba hilo ambako uchunguzi wa Takukuru umebaini eneo hilo si mali ya wakulima hao wala Okash bali ni Halmashauri ya Meru na lilitengwa na serikali kwa ajili mradi wa Malula Industrial na walalamikaji wa pande zote mbili wamejulishwa juu ya uchunguzi huo.

Chanzo: habarileo.co.tz