Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waiba vifaa vya ujenzi daraja la JPM

Polisi Mwanza Ujenzi Jpm Waiba vifaa vya ujenzi daraja la JPM

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kuiba vifaa vya ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi maarufu kama daraja la JPM.

Vitu hivyo ni pamoja na mashine 7 za kuchomelea, stick za kuchomelea vyuma, welding cable na Drilling bit mbili ambavyo hadi sasa thamani yake bado haijafahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amewataja watu hao kuwa ni Halfan Seif ambae ni fundi nondo, Humfrey William nae ni fundi pamoja na mlinzi aitwae Bwire Manyama, ambao wanadaiwa kushirikiana kuviiba vifaa hivyo kisha kuvificha kwenye nyumba iliyopo jirani na linapojengwa daraja hilo kisha kujaribu kuvisafirisha kwa kutumia gari aina ya toyota Noah nyeusi yenye namba za usajili T 707 BPG ambayo nayo inashikiliwa.

Aidha kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na kasmba ukikamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani huku akiwaonya watu wengine watakaojaribu kuiba vifaa vya ujenzi wa daraja hilo kwa kusema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live