Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahuni wavamia kanisani, waiba Rolls Royce la Askofu na mabilioni

Poesoo Wahuni wavamia kanisani, waiba Rolls Royce la Askofu

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhubiri anayejulikana kwa mtindo wake wa maisha ya ufahari ameibiwa vito vya thamani ya zaidi ya $1m (zaidi ya Bil. 2.3) wakati wa mahubiri yaliyopeperushwa moja kwa moja katika jiji la New York.

Lamor Whitehead, 44, ameapa kwamba wahalifu "hawataepuka"

Miongoni mwa vitu alivyoibiwa, mhubiri huyo anayeendesha gari aine ya Rolls Royce ni saa aina ya Rolexes, almasi na zumaridi.

Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Mpaka sasa hakuna mshukiwa ambaye ametajwa wala kukamatwa.

Katika video hiyo Bw Whitehead anasikika akiuliza "Ni wangapi kati yenu mmepoteza imani kwa sababu mliona mtu mwingine akifa?" muda mfupi kabla ya watu kadhaa waliovalia nguo nyeusi kuingia kanisani huko Brooklyn.

"Nilipowaona wakiingia kwenye hekalu na bunduki zao, nilimwambia kila mtu [alale] chini, kila mtu alale," baadaye alisema kwenye ukurasa wa Instagram.

"Sikujua kama walitaka kulipiga risasi kanisa au kama walikuwa wanakuja kwa wizi."

Kulingana na Bw Whitehead, wezi hao waliojifunika nyuso zao walitoroka kwa kutumia gari aina ya Mercedes.

Kufuatia wizi huo, gazeti la New York Post liliripoti kuwa vitu vilivyochukuliwa kutoka kwake na mkewe ni pamoja na saa za Rolex na Cavalier za $75,000, rubi ​​ya Episcopal ya $25,000 na pete ya almasi na pete za $25,000 - na hata pete yake ya harusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live