Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahukumiwa kwa kuzamia Afrika Kusini

HUKUMU Wahukumiwa kwa kuzamia Afrika Kusini

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaamuru kulipa faini ya shilingi 70,000 au kwenda jela miaka miwili raia 28 wa Tanzania baada ya uwatia hatiani kwa kuingia Afrika Kusini kinyume na sheria za uhamiaji.

Wakili wa Serikali Idara ya Uhamiaji, Shija Sitta amesema kuwa watuhumiwa hao walirejeshwa nchini Agosti 20 mwaka huu kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere baada ya kugundulika wameingia Afrika Kusini kinyume cha Sheria.

Hakimu Mkaazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi amesema watuhumiwa wote wamekiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live