Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahitimu vyuoni bado walia rushwa ya ngono

9a5f636409acb42b81c14d26b06e3a2a Wahitimu vyuoni bado walia rushwa ya ngono

Tue, 15 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADHI ya wanafunzi wakazi wa Tanga waliohitimu vyuo vikuu nchini, wamesema kuwa ili kuondoa rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni, juhudi kubwa inahitajika kutoka kwa wadau wa elimu, serikali na wanafunzi wenyewe.

Wamefafanua kuwa rushwa ya ngono vyuoni, inakithiri kila siku lakini kutokana na mazingira inakuwa ni vigumu kuikemea licha ya kuonekana waziwazi.

Wakizungumza na HabariLEO jijini Tanga kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanafunzi waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Chuo Cha Uongozi wa Fedha(IFM) na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, walibainisha kuwa wanafunzi wengi wa kike wanatumbukia katika rushwa ya ngono kwa kulazimishwa ili waweze kufaulu katika mitihani na majaribio ya chuo.

"Kwa sisi wanafunzi wa kike mpaka ukimaliza chuo hujatongozwa na mwalimu unashukuru Mungu, lakini wengi wanatoka na wahadhiri si kwa kupenda ila yatakayokupata utajijua mwenyewe,"alisema Shukuru Hamidu.

Jesca Isaya aliyekuwa akichukua Shahada ya Sayansi Kilimo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibainisha kuwa wakati mwingine kama umetongozwa na mhadhiri halafu ukakataa, matokeo yake unafelishwa mitihani bila sababu au usajili wako unajikuta unasumbua Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

"Mimi nafikiri kuna haja serikali ikafuatilia kwa makini na kuchukua hatua kali dhidi ya walimu wakware, mfano kuna rafiki yangu tumehitimu naye mwaka juzi alitongozwa na mhadhiri akataa akajikuta masomo manne kawekewa 'Supplementary' wakati alifaulu, kwa hiyo ni mazingira magumu," alisema.

Hamisi Abubakari alisema mpenzi wake wa kike waliyesoma wote Shahada ya Teknolojia ya Habari UDOM, alijikuta akitumiwa ujumbe mfupi wa simu aachane naye la sivyo mitihani yake yote atafeli.

Haruna Jamal mwalimu mstaafu ambaye amefundisha vyuo vya kati binafsi katika fani ya afya, uuguzi kwa miaka mingi, alisema kuwa suala la rushwa ya ngono kati ya walimu na wanafunzi limekuwa ni tatizo sugu la chinichini ambalo linachukuliwa jambo la kawaida, lakini waathirika wakubwa ni wanafunzi.

Chanzo: habarileo.co.tz