Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji wanne wadakwa Kilimanjaro

58326 Pic+wahamiaji

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Idara ya uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro  imewakamata raia wanne wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia Tanzania kinyume na sheria.

Raia hao wamekamatwa juzi katika mpaka wa Holili wakitumia njia za panya huku wakiwa na vitambulisho vikionyesha ni raia wa Ethiopia na hati za kusafiria za Kenya zenye mihuri bandia.

Akizungumza leo Jumamosi Mei 18, 2019 mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, Albert Rwelamira amesema watu hao wanafanya idadi ya waliokamatwa hivi karibuni kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa na hati za kusafiria zenye mihuri bandia kufikia 10.

“Uchunguzi umebaini watu hawa ni raia wa Ethiopia na hati zao za kusafiria za Kenya  walizokutwa nazo walitengenezwa na mawakala katika  kituo cha Gambo mpakani mwa Kenya na Ethiopia.”

“Walikabidhiwa zikiwa zimegongwa mihuri inayoonyesha tayari wametoka Kenya kupitia kituo cha Taveta na kuingia Tanzania kupitia kituo cha Holili,” amesema Rwelamira.

Amebainisha kuwa siku za hivi karibuni raia wa Ethiopia na Somalia wamekuwa wakiingia Tanzania wakiwa na hati zenye mihuri bandia na wamefanya uchunguzi na kubaini mawakala wanaowasafirisha raia wa nchi hizo ndio wanaowagongea mihuri hiyo nje ya mpaka wa Tanzania.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz