Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu wadakwa wakijifanya wachezaji Coastal Union

Mbaroni Wahamiaji haramu wadakwa wakijifanya wachezaji Coastal Union

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Tanga, limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wanne raia wa Cameroon, ambao wamedai wapo nchini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na timu za Coastal Union na African Sports zilizopo jijini Tanga.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Kagimbo Bakari amesema wahamiaji hao wamedai wameletwa na wakala aitwaye Benard Matomondo Mfaume na kwamba waliingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) na kupata visa ya matembezi (HV) za siku 90, badala ya visa za kibiashara (BV) kulingana na shughuli walizokuja kuzifanya.

Hata hivyo alibainisha kuwa mara baada ya kuwakamata raia hao, waliwaita viongozi wa timu za African Sports na Coastal, ambao walikana kuwatambua wala kuwa na mawasiliano nao na barua walizokuwa nazo zote ni za kughushi na pasipoti walizokuwa nazo sio sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live