Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahamiaji haramu 61 wakamatwa wakisafirishwa kwenye lori (+video)

Screenshot 2021 01 14 At 12.58.35 660x400.png Wahamiaji haramu 61 wakamatwa wakisafirishwa kwenye lori (+video)

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, limewanasa wahamiaji haramu 61 raia wa Ethiopia wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi kwa kutumia lori la mizigo huku dereva wa gari hilo pia akishikiliwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji hao.

Akizungumza na wandishi wa habari katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Mbeya, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jerome Ngowi, amesema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kizuizi cha magari kilichopo kijiji cha Gari Jembe barabara Kuu ya Tanzania na Malawi.

Amesema wahamiaji haramu hao walikuwa wamefichwa kwenye lori aina ya Scania yenye namba za usajili T. 509 AZZ ambalo lilikuwa linaendeshwa na dereva ajulikanaye kwa jina la Rabdi Ramadhani (48) mkazi wa Unga Limited mkoani Arusha.

Chanzo: millardayo.com